Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

August 18, 2018

June 12, 2018

KAMPUNI ZITAKAZOLETA UBABAISHAJI KATIKA MALIPO YA PAMBA YA WAKULIMA KUFUTIWA LESENI

NA TIGANYA VINCENT
RS TABORA
 SERIKALI imesema haitasita kuzifuta na kuzinyang’anya leseni Kampuni ambazo zinanua pamba hapa nchini ikiwa zitachelewesha fedha za wakulima  wa zao hilo na kuanza kuwazungusha bila kuwalipa fedha zao.
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Kilimo Dkt Charles Tizeba wakati akizindua ununuzi wa Pamba katika Kijiji cha Muhilidede wilayani Uyui Mkoani Tabora
Alisema ni jukumu la Kampuni zinapomaliza kununua pamba ya mkulima kumlipa palepale siku hiyo hiyo kwa kuwekea fedha katika Akaunti yake au kupitia simu ya mkononi na kisha pesa ikishaingia anaone ujumbe wa kumhakikisha kulipwa
Waziri huyo aliwataka Viongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika, Halmashauri za Wilaya na Wakulima walisikubali Kampuni ziondoe pamba katika Vituo vya kununulia pamaba kama malipo kwa wakulima hajafanyika na chama cha mshingi na Halmashauri hazijalipwa.
Dkt. Tizeba alisema Serikali inaachukua hatua hiyo ili kurejesha imani kwa wakulima juu ya ushirika ambao umekuwa ukipigwa vita na baadhi ya watu.
Aidha Waziri huyo aliwaagiza Viongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika kuhakikisha vinawakamata na kuwapeleka Polisi watu wote ambao watapeleka pamba iliyochanganywa na uchafu na ile wekewa maji kwa sababu watu hao ni sawa na wezi.
Alisema mkulima anaweka maji kwenye pamba na yule anayeweka uchafu anataka kuhujumu zao hilo  kwa kusababisha mbegu zitakazolishwa zisiote na wanunuzi watoe bei mbaya kwa pamba chafu.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri aliwataka viongozi wa Vyama vya Ushirika kutumia sehemu ya asilimia 33 ya kila kilo watakayopata kununua Matrekta ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo msimu ujao.
Alisema kuwa kupitia kilimo cha matumizi ya jembe la mkono hakiwezi kuleta mapinduzi ya kilimo na manufaa kwa mkulima mkoani humo.
Mwisho

DK. MNDOLWA: MNASHINDWAJE KULIPA ADA YA UANACHAMA YA KILA MWAKA AMBAYO GHARAMA YAKE NI SAWA NA SODA MOJA?

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa akizungumza na Viongozi wa Jumuiya hiyo, leo mjini Tarime mkoani Mara. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Erasto Sima, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo mkoa wa Mara Samweli Kiboya na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania uoande wa Zanzibar Haidar haji Abdallah na kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara Mrida Mshota.

Na Bashir Nkoromo, Tarime
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa ameshangazwa na baadhi ya wanachama wa CCM na Jumuiya zake kushindwa kulipa ada ya uanachama ya sh. 1200 kwa mwaka, ambayo ni sawa ya bei ya soda moja.

Dk. Mndolwa ameelezea kushangazwa huko, wakati akizungumza na viongozi wa CCM na Jumuiya za CCM kutoka Wilaya za mkoa wa Mara, katika ukumbi wa CMG mjini Tarime, leo, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani humo.

Kufuatia hali hiyo Dk. Mndolwa ameagiza viongozi kusimamia ipasavyo ili kuhakikisha kila mwanachama wa CCM na Jumuiya ya Wazazi Tanzania analipa ada yake ya kila mwezi, akisisitiza kuwa watakaoshindwa kufanya hivyo itakuwa ni mfano unaoonyesha kuwa hawafai uongozi kutokana na kushindwa kusimamia  uhai wa Jumuiya hiyo na Chama Cha Mapinduzi.

"Unamkuta mtu kila mara anajinasibu kuwa ni mwanachama wa CCM au Jumuiya ya Wazazi, lakini wakati huo huo halipi ada ya uanachama ya kila mwaka mbayo gharama yake kwa kila mwaka ni sawa na bei ya soda moja ambayo kila siku anamudu kuinunua", alisema Dk. Mndolwa.

Alisema, ni jambo la muhimu kwa kila mwanachama kuhakikisha analipa ada yake ya uanachama kwa sababu kufanya hivyo ndiyo ishara pekee inayodhihirisha uanachama wake kwa kuwa asipofanya hivyo anakuwa mwanachama mfu asiyeshiriki katika kuimarisha uhai wa Chama.

Dk. Mndolwa amewasisitiza wanachama wa CCM kujiunga na Jumuiya za Chama akisema kwamba kufanya hivyo kunatoa fursa pana zaidi kwa mwanachama kuijenga CCM na pia hata kuwea kupata nafasi za uongozi kwa wepesi zaidi kuliko akiwa mwana CCM tu.

"Tazameni, hivi sasa mimi ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM lakini ni kwa sababu nimekuwa mwanachama wa Jumuiya ya Wazazi na kisha nikagombea kupitia huko na kupata Uenyekiti wa Jumuiya hii ambapo sasa kwa nafasi niliyo nayo ya Uenyekiti nimekuwa pia Mjumbe wa Kamati Kuu", alisema Dk. Mndolwa.

Akizungumzia maadili katika jamii, Dk. Mndolwa aliwatupia lawama wazazi kuwa ndiyo chanzo kikubwa cha kumomonyoka kwa maadili katika jamii kutokana na kuwaacha watoto wao kufanya wapendavyo katika masuala ya tabia.

"Unakuta binti anatoka nyumbani amefaa nguo za kubaka maungo na zinazoacha wazi baadhi ya maungo yanayostahili kusitiriwa, mzazi anaona lakini anamuacha bila kumkemea, matokeo yake binti anakuwa mitaani katika namna ya kutokuwa na maadili bora, ikitokea hivyo jua lawama ni kwa mzazi", alisema Dk. Mndolwa.

Alisema, hali kadhalika ni kosa la mzazi pale mtoto wa kiume anapotoka nyumbani huku amevaa katula au suruali inayoporomoka matakoni, kwa sababu mzazi anapaswa kukemea uvaaji huo kwa kuwa unatia aibu katika jamii.

"Unakuta mzazi anampa hela nyingi mtoto wakati anakwenda shuleni  huku akisema kuwa kwa kuwa yeye alisoma katika mazingira ya taabu hataki mwanae asome kwa taabu, kumbe hajui kuwa kwa kufanya hivyo anamjengea mtoto vishawishi vya kutumbukia katika utumiaji wa dawa za kulevya na uvutaji bangi", alisema Dk. Mndolwa.

Dk. Mndolwa aliwataka wazazi kuwa mstari wa mbele kuwahakikisha wanasaidia kujenga maadili ya jamii kwa kuwakanya na kuwachukulia hatua thabiti watoto wao kila wanapowagundua au kuwaona wanajaribu kuanza kuiga tabia zinazomomonyoa maadili.

Akizungumzia mshikamano ndani ya Chama, Dk. Mndolwa aliwataka wana CCM kuachana kabisa na mtindo wa kung'ang'ania makundi kila baada ya uchaguzi na pia kuachana na tabia ya kuthani mtu fulani ni maarufu kuliko chama.

Dk. Mndolwa alisema, ikiwa wanachama wataachana na mambo hayo CCM inakuwa imejihakikishia kupata ushindi kila uchaguzi kwa kuwa inao wanachama na wapenzi wengi na kinachohitajika ni mshikamano tu.

"Hadi sasa kuna baadhi ya majimbo au Kata walizoshinda wapinzani katika uchaguzi uliopita, lakini kwa maoni yangu wapinzani hawakushinda maeneo hayo eti kwa sababu ni weledi sana, hapana. ukweli ni kwamba walishinda kwa sababu ya uzembe wa wana CCM wenyewe kung'ang'ania makundi baada ya kura za maoni", alisema Dk. Mndolwa.

Lengo la ziara hiyo ya Dk. Mndolwa katika mikoa ya Kanda ya ziwa na mkoa wa Singida, ni kuwashukuru wananchama wa Jumuiya ya Wazazi kwa kumchagua kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo na pia kuwatambulisha Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania kwa upande wa Zanzibar Haidar  Haji Abdallah na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Erasto Sima ambao ameambatana nao katika ziara hiyo. 

Korea Kaskazini na Marekani: Donald Trump na Kim Jong Un wakutana ana kwa ana Singapore

US President Donald Trump (R) shakes hands with North Korea"s leader Kim Jong-un (L) as they sit down for their historic US-North Korea summit

Haki miliki ya pichaAFP
Mkutano wa kihistoria kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un umefanyika nchini Singapore.
Wawili hao walikutana kwanza kwa dakika 38 kwa mujibu wa ikulu ya White House, na walikuwa ni wawili hao pekee na wakalimani wao.
Mkutano huo ulianza kwa viongozi wawili kusalimiana kwa tabasamu na kisha kuelekea ukumbi wa maktaba ya Cappela Hotel kwa ajili ya sehemu ya kwanza ya mkutano wa ana kwa ana baina yao.
Bw Trump amesema wawili hao walipiga hatua kubwa na kwamba karibuni kutakuwa na sherehe ya kutia saini nyaraka ya makubaliano.
Wamekuwa wakijadiliana kuhusu njia za kupunguza uhasama rasi ya Korea na kati ya Korea Kaskazini na Marekani na pia jinsi ya kupunguza silaha za nyuklia.
Hata hivyo, haijabainika ni nini kitakuwepo kwenye waraka ambao watautia saini.
Trump alisikika akisema kuwa anatarijia makubaliano mazuri katika mkutano huku Kim akisema kuwa haikuwa rahisi kufika hapo.
Mkutano uliokua ukisubiriwa kwa hamu na ghamu ulifanyika katika Hotel ya Capella katika kisiwa cha utalii cha Sentosa.
Trump and KimHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWawili hao wakitembea katika hoteli ya Capella, Singapore
Viongozi hawa wakiingia katika mkutano walionekana wenye tabasabu, na kusalimiana kwa kushikana mikono, na baadae Kim Jong Un alimshika bega Trumpa kisha wakaanza kuzungumza kwa msaada wa wakalimani wao.
Baadaye washauri na maafisa mbalimbali walitarajiwa kuingia kuendelea na mkutano huku suala la nyuklia likitarijiwa kujadiliwa kwa kina na haijajulikana bado makubaliano yatakua yapi.
Akizungumza kabla ta mkutano , katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Antonio Guterres amesema kuwa umoja wa mataifa utatoa msaada wowote wa kuhamasisha makubaliono katika mkutano huo.
''Viongozi wawili, wanajaribu kujadiliana jinsi ya kufikia makubaliano ambayo yalileta sana utata mwaka jana, amani na suala la kusitisha nyuklia ndio vinabaki kuwa lengo kuu, kama nilivyowaandikia mwezi uliopita kutahitajika ushirikiano wa hali ya juu na kutakua na changamoto za hapa na pale katika makubaliano, Marekani wanatakiwa kusimamia kwa vyovyote," alisema Guterres.
Kim arrives at summit venueHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBw Kim alipokuwa anawasili hoteli ya Capella,Sentosa
Mcheza kikapu wa zamani wa NBA, Dennis Rodman amefika Singapore asubuhi ya leo kwa ajili mkutano huo, Rodman ambaye ni rafiki wa kiongozi wa Korea Kaskazini amesema kuwa anafurahia kufika na kushuhudia mkutano huo wa kihistoria.
Mkutano huu unaweza kuwa na mafanikio
Uhusiano wa viongozi hawa wawili umepitia kwenye milima na mbonde kwa kipindi cha miezi 18 iliyopita, wakirushiana matusi na kutishiana vita kabla ya uhusiano wao kuchukua mkondo mwingine na kuamua wawili hao kukutana.
MkutanoKwa nini hatua hii imefikiwa hivi sasa?
Mwaka wa kwanza wa Trump katika kiti cha urais ulianza kwa mvutano mkubwa na kurushiana maneno huku Kim naye akiendeleza majaribio ya silaha za nuklia na kukiuka ilani ya kimataifa.
Rais wa Marekani aliapa kupambana ikiwa Pyongyang itaendelea kuitishia Marekani, wote wakipeana majina ya kukebehi.
Korea Kaskazini iliendelea kukaidi na kufanya jaribio la nuklia la sita mwezi Septemba mwaka 2017.
Baadae Kim alitangaza kuwa nchi yake imefanikiwa mpango wake wa kua taifa la nuklia, likiwa na silaha zinazoweza kuifikia Marekani.
Lakini mwanzoni mwa mwaka 2018, Korea Kaskazini ilianza kuboresha mahusiano na Korea Kusini kwa kupeleka timu na ujumbe kwenye michuano ya Olimpiki mjini Pyeongchang.
Mwezi Machi, Donald Trump aliushangaza ulimwengu kwa kukubali mwaliko kutoka kwa Kim wa kukutana ana kwa ana.
Tangu wakati huo, njia ya kuelekea mkutano huu ikawa yenye changamoto, Trump akiahirisha kabisa.Lakini sasa viongozi hao watakaa pamoja.
Singapore ni nchi ya tatu ambayo Kim Jong-un ameitembelea tangu alipokuwa Kiongozi mwaka 2011.
safari yake ya kwanza ilikuwa nchini China mwezi Machi na mwezi Aprili akawa kiongozi wa kwanza wa Korea Kaskazini kutembelea Korea Kusini ambapo alikutana na Moon Jae-in.

Kamati ya watu wenye ulemavu Rukwa kutekeleza agizo la Waziri Mkuu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Watu wenye Ulemavu Mkoa wa Rukwa Lt.Col. John Antonyo Mzurikwao akiendesha kikao chake cha kwanza cha kamati hiyo tangu kuteuliwa kwake na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa mwezi wa tano mwaka 2018.
...............................................................................................................................................................
Kamati ya watu wenye ulemavu Mkoa wa Rukwa imeaswa kuhakikisha inawatambua watu wenye ulemavu na kubaini mahitaji yao pamoja na kuona namna ya kutatua changamoto zao ili kuweza kuwasaidia katika kufikia malengo yao katika sekta mbalimbali za kimaendeleo.
“Katika Mkoa wa Rukwa tunachamoto kubwa juu ya namna ya kuwahudumia watu wenye ulemavu, kwani mara nyingi watu hawa wamekuwa wakileta malalamiko yao katika ofisi hii, hivyo uwepo wa kamati hii utapunguza sana changamoto wanazokabiliana nazo ndugu zetu hawa.”Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo alipokuwa akizindua kamati ya watu wenye ulemavu ngazi ya Mkoa.
Ameongeza kuwa ni matumaini ya serikali kuwa kamati hiyo itazisimamia kamati zote zilizopo chini yake kuanzia ngazi ya halmashauri, mitaa na vijiji ili kujua idadi ya watu wenye ulemavu kuanzia ngazi ya kitongoji hadi kufikia ngazi ya halmashauri na kupeleka taarifa ya utekelezaji wa majukumu yao kwa Ofisi ya Rais TAMISEMI.
Kwa upande wake akisoma taarifa ya kamati katibu wa kamati ya watu wenye ulemavu mkoa Godfrey Mapunda amezitaja changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na kutokuwa na taarifa sahihi juu ya haki zao, kutokuwepo kwa miundombinu isiyozingatia hali za watu wenye ulemavu zinazowapelekea kushindwa kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za kijamii pamoja na Imani potofu kwa jamii inayowapelekea kushindwa kupata elimu na mahitaji muhimu.
Na kueleza majukumu ya kamati hiyo ikiwa ni pamoja na “Jukumu la kwanza itakuwa ni kutambua haki na uwezo wa watu walio na ulemavu katika mkoa lakini pia kuwasaidia watu wenye ulemavu na familia zao na kupanga mipango yenye ufanisi ili kupunguza umasikini kupitia shughuli za kujiingia kipato, kuratibu shughuli zote za watu wenye ulemavu katika mkoa, kulinda na kukuza ustawi wa watu wenye ulemavu katika Mkoa,” Alisema.
Hadi kamati hiyo inazinduliwa na Mkuu wa Mkoa asilimia 42 ya kamati za watu wenye ulemavu kuanzia ngazi ya Kijiji hadi halmashauri zilikuwa zimeshaundwa na walemavu 774 wamebanika huku maazimio ya kamati hiyo ikiwa ni kuhakikisha kamati zinaundwa kwa asilimia 100 na walemavu wote kutambulika na kuwa na takwimu sahihi ili kuweza kuwafikishia huduma stahiki.
Hii ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa alilolitoa alipohudhuria hafla ya chakula cha mchana kwa watu wenye ulemavu iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya IPP, Bw. Reginald Mengi kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee mapema mwezi wa pili mwaka 2018.


June 11, 2018

MWENYEKITI WA CCM MKOA WA IRINGA AWAPA ONYO KALI WANA CCM KILOLO ATAKA MBUNGE MWAMOTO NA MADIWANI WASIINGILIWE ....

Mwenyekiti  wa  CCM  mkoa wa  Iringa Albart Chalamila  akizungumza na wajumbe wa Halmashauri  kuu ya CCM wilaya ya  Kilolo  leo 
Viongozi  wa  CCM  wilaya na mkoa  wa Iringa  wakiimba  wimbo wa  chama kabla ya  kuanza  kikao cha Halmashauri  kuu wilaya  leo 
Mwenyekiti wa CCM  mkoa  Albart Chalamila  kulia  akishuhudia  wana CCM  Kilolo wakimpokea kwa shangwe  leo 
Wajumbe  wa Halmashauri  kuu ya   CCM kilolo  wakidua 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Albart Chalamila  akisisitiza jambo 
Mkuu  wa wilaya ya  Kilolo  Asia  Abdalah  akieleza changamoto za usafiri Kilolo 
Mbunge wa  Kilolo  Venance  Mwamoto  akitoa kero za  wana Kilolo na mafanikio mbali mbali yaliyofikiwa katika  jimbo  hilo mbele ya mwenyekiti wa CCM mkoa 
Mwenyekiti  wa CCM mkoa wa Iringa Albart Chalamila  akipokelewa kwa heshima  kubwa  Kilolo 
Mwenyekiti wa CCM mkoa  akivishwa  skafu baada ya  kupokelewa  Kilolo leo 
Viongozi wa  CCM mkoa wa Iringa wakiongozana na  mwenyekiti wa CCM mkoa Albart Chalamila  na katibu wa CCM mkoa Christopher Mgala  kukagua  gwaride la  UVCCM 
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa,Christopher Magala akiwataka  makatibu  kufanya  usajili wa  wanachama 
Baadhi ya  wajumbe wa Halmashauri  kuu ya  CCM Kilolo  wakiwa katika  kikao  leo 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Viti 15 Bara), Theresia Mtewele akitoa  salam zake kwa  wana CCM 
Mbunge wa  Kilolo  Venance Mwamoto  kulia  akimkabidhi  zawadi ya  mbuzi mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Albart Chalamila kwa niaba ya wajumbe wa Halmashauri kuu ya  CCM Kilolo 
Mwenyekiti wa CCM  mkoa wa Iringa Albart Chalamila  akiwa amebeba  mbuzi  aliyopewa  zawadi  na  wajumbe wa Halmashauri  kuu ya  CCM Kilolo leo 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Albart Chalamila  kulia  akimkabidhi  cheti  mkuu wa  wilaya ya  Kilolo  Asia  Abdalah  kutokana na  kuwa karibu wa CCM 
Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo  Asia Abdalah  akipongezwa na mwenyekiti wa  wilaya ya  Kilolo Kilian Myenzi mara  baada ya kukabidhiwa  cheti  cha pongezi na  mwenyekiti wa CCM mkoa 
Mwenyekiti wa  CCM  Kilolo  Kilian Myenzi  akimkaribisha mwenyekiti wa  CCM  mkoa wa Iringa 
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Albert Chalamila amewaonya  wanachama wa chama  hicho  wilaya ya  Kilolo   kuepuka  kuanza kampeni za  udiwani na ubunge kabla ya  wakati .

Kuwa  CCM hakitamfumbia  macho wanachama  yeyote  ambaye atajihusisha na mbio  za udiwani ama ubunge katika jimbo hilo la Kilolo ambalo mbunge wake ni Venance Mwamoto .

“Huku nyuma kulikuwepo na baadhi ya wana CCM waliokuwa wakijinasibu kwamba wao ndio wenye chama na wana uwezo wa kuamua lolote bila maamuzi ya vikao vya chama kwa muda mrefu wana CCM hao walionekana watu wenye nguvu kuliko chama, nataka kuwaambia CCM ya sasa sio ya wakati ule, tunawasubiri wapiti kwenye reli, tuwashughulikie,” 

Chalamila  alitoa onyo hilo kali kwa  wana CCM kupitia wajumbe wa Halmashauri  kuu ya  CCM wilaya wakati wa  kikao  cha halmashauri kuu ya CCM ya wilayani hapo  leo .

Katika  kikao   hicho  ambacho ni mwendelezo wa vikao kama hivyo katika wilaya mbali mbali za  mkoa wa Iringa kikao cha kazi kwa ajili ya kuelezea mwelekeo wake wa usimamizi wa shughuli za chama katika kipindi cha uongozi wake tangu ashike wadhifa huo mwishoni mwa mwaka jana.

Alisema  kuwa tayari  amekwisha  jipanga yeye kwa  kushirikiana na vyombo  mbali mbali  za  kiusalama ndani ya  chama  kuweka  mtego wa  kuwabaini wanachama  walioanza kampeni na wasilalamike  watakapochukuliwa hatua kali .


" Tayari  nimeanza  kufanya uchunguzi kwa  wale  ambao  wanajipitisha katika kata na  jimbo la Kilolo kwa  ajili ya uchaguzi mkuu ujao narudia  tena  wakibainika  wanachama  hao  nitawapokonya kadi na kuwasimamisha  kujihusisha na  shughuli  yeyote  ya  chama "

Mbali ya  kutowataja majina wanachama hao  Chalamila aliwataka wana CCM hao kujitafakari na kama  wana ndoto  za  kuja kugombea wasitegemee tena kwani pindi  watakapobainika  watafukuzwa  chama .


Kwani  alisema baadhi ya  wana CCM  wanaoshiriki kuhatarisha amani ndani ya chama hicho ni wale waliopewa dhamana ya kuwa wajumbe wa vikao vikubwa vya chama  na kuwataka  kuachana na tabia   hiyo .

“Nasema Mwacheni  mbunge  Venance Mwamoto na madiwani wote wa Kilolo wafanye kazi ya kuwatumikia wananchi kwa amani na utulivu  ili mbunge na madiwani  wamalize  miaka yao mitano bila kuingiliwa na mtu "


 Chalamila alisema makundi ndani ya  chama hayana nafasi na  kuwa visasi na mioyo ya kinyongo miongoni mwa wana CCM wakati na baada ya chaguzi za chama na jumuiya zake jambo ambalo limekuwa likisabisha mpasuko wa muda mrefu ndani ya chama hivyo ni lazima yaachwe na  wasioacha  watawajibika .Aliwataka wenye taarifa za wanachama wenye mienendo mibaya na inayotishia uhai wa chama waziwasilishe kwa kuzingatia taratibu, kanuni na katiba ya chama ili ziweze kufanyiwa kazi.

Kuhusu  mwelekeo wake  katika uongozi wake kuwa ni kuendesha chama kwa kuzingatia msingi wa siasa safi zisizo na majungu ili kulinda taswira ya mkoa wa Iringa ulioharibiwa na siasa za majungu hasa  kipindi cha nyuma kabla yake .
Aidha  amewataka  wana CCM kujiandaa kwa uchaguzi wa mwakani wa Serikali za Mitaa  na  kuwa ni  uchaguzi muhimu unaosaidia kutathimini utekelezaji wa Ilani ya chama kwa kuzingatia vipaumbele vyake na ndio unatoa dira ya maandalizi ya uchaguzi mkuu wa 2020.

Hata  hivyo  mwenyekiti  huyo  alimpongeza mkuu  wa wilaya ya  Kilolo Asia  Abdalah na  viongozi wa CCM wilaya  hiyo kwa  kufanya kazi kama  timu  moja na  kuwa  toka ameanza  ziara  yake  Kilolo ni wilaya ya pekee  kukutana na  mkuu wa  wilaya na mbunge wa jimbo .

Katika hatua  nyingine  mwenyekiti huyo wa  mkoa amewataka   wajumbe wa Halmashauri  kuu ya  CCM wilaya na  viongozi  kuendelea  kutoa  elimu kwa wananchi  kuacha kuuza  ovyo ardhi huku  akipongeza uamuzi wa mkuu wa wilaya ya  Kilolo  kuzuia uuzaji kiholela  ardhi  yenye ukubwa wa  zaidi ya  ekari 4500.

Kwa upande wake  katibu wa CCM mkoa wa Iringa Christopher Mgalla aliwataka  watendaji wa CCM ngazi zote  kuhakikisha  wanasajili  wanachama kupitia mfumo rafiki  utakaokwenda sanjari na  sayansi na Teknolojia  ili  kuwezesha  mwenyekiti wa chama Taifa  kuongea na mwanachama  yeyote pindi anapohitaji akiwa Ikulu .

Hivyo  alisema  suala la uhai wa chama ni  vizuri  kwenda sambamba na  ulipaji wa ada  na usajili wa wanachama  wote .


Huku mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Viti 15 Bara), Theresia Mtewele aliwataka  wana  CCM hasa  wajumbe wa Halmashauri  kuu  kuendelea  kufanya kazi ya  kukijenga  chama badala ya  kukiingiza  chama katika makundi ambayo  yamekuwa  yakihatarisha  uhai wa chama .

Alisema  ndani ya CCM wanachama  wote  wanawajibu wa  kukijenga chama na  kuwa ni lazima katiba na  kanuni za  chama  kuzingatiwa  katika  uendeshaji wa chama .


Mkuu  wa  wilaya  ya  Kilolo  akieleza  utekelezaji wa ilani ya  CCM katika  wilaya  hiyo alisema  anaipongeza  serikali ya  awamu ya tano chini ya Rais Dkt  John  Magufuli kwa kuendelea  kuharakisha maendeleo ya  Kilolo  hasa kwa  kuahidi  kushughulikia  changamoto ya  barabara ya Iringa - Kilolo .

Kuwa  kero  hiyo ya  barabara  hadi 2025   wanategemea  Kilolo  kuwa na lami  na  hivyo wananchi  wataondokana na kero   hiyo .

 Wakati  mbunge wa  jimbo la  Kilolo Venance Mwamoto pamoja  na  kumpongeza  mwenyekiti  huyo kwa  ziara  yake Kilolo  bado  alisema  ziara ya Rais ndani ya  wilaya ya  Kilolo  imeleta  matunda  kwa  wilaya  hiyo na kuwa tayari  serikali imetoa  pesa  za  miradi ya maji Ilula  na  kero ya maji  inaendelea  kufanyiwa kazi .

Pia  alisema ujenzi wa Hospitali ya  kisasa  ya  wilaya ya  Kilolo kilikuwa ni  sehemu ya  kilio  kwa wananchi wa Kilolo  ila  sasa ujenzi huo unaendelea  na  serikali ya Dkt Magufuli  imeahidi  ujenzi huo kumalizika haraka  zaidi .