Thursday, November 5, 2009

AJALI IRINGA; KAMPUNI YA MABASI YA HOOD YASHINDWA USHINDANI YAANZISHA VURUGU BARABARANI















Askari wa usalama barabarani mkoa wa Iringa wakipima eneo la ajali baada ya Tax iliyokuwa ikitumiwa na ndugu wa mwanafunzi Rehema Ismail ambaye mmoja kati ya wanafunzi wawili wa VETA Iringa aliyeuwawa kwa kupigwa risasi wakitoka kuzika eneo la Mlowa mjini Iringa leo katika ajali hiyo watu wawili wamejeruhiwa

Pia katika ajali ya pili iliyotokea usiku huu katika mlima wa Ipogolo mjini hapa basi la kampuni ya Hood limeligonga kusudi basi la Sumry ambalo pia linafanya safari zake kati ya Mbeya na Arusha ,Hood limeanza vurugu hizo kutokana na kushindwa kumudu ushindani wa kibiashara

Abiria waliokuwemo katika basi la Hood wameieleza blog hii kuwa dereva wa Hood toka wakiwa njiani alikuwa akimtishia dereva wa Sumry kuwa itakuwa vigumu kwake kufika Mbeya bila kusababishiwa ajali vitisho ambavyo vimetimizwa mjini Iringa.

Katika tukio hilo la ajali hakuna aliyepoteza maisha wala kupata majeraha ya kutisha.

Habari hii utaisoma katika gazeti la Tanzania Daima jumamosi

0 comments: