Kufuatia ajali hiyo Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Magungu Dokta RASHID SAID amethibitisha kutokea kwa vifo Viwili vya askari polisi huku akisisitiza kuwa hali za askari Wanne waliojeruhiwa katika ajali hiyo bado si nzuri.
Mwandishi wa habari wa Uhuru FM aliyekuwepo kwenye msafara huo amesema msafara huo ulikuwa unatokea Wilayani Lushoto kwenda Hale Wilayani Korogwe kwa ajili ya mapumziko ya Makamu wa Rais ambaye yupo Mkoani Tanga kwa ajili ya ziara ya kikazi.
Gari lililohusika katika ajali hiyo ni lenye namba za usajili PT-2000 ambalo lilikuwa nyuma ya msafara huo wa Makamu wa Rais.
Miili ya askari hao waliokufa imehifadhiwa katika Kituo cha Afya cha Magungu.
0 Maoni:
Post a Comment