January 24, 2012

NIMEPITA MOROGORO SAA 4 ASUBUHI HII SIJAPENDEZWA NA UTARATIBU WA UCHIMBAJI DAWA VICHAKANI

UTARATIBU huu wa mabasi ya abiria kusimama Porini ili abiria waweze kuchimba dawa binafsi sijaupenda Kabisa Kwani katika mabasi watu husafiri na wakwe zao ama watoto zao sasa huu utamaduni wa Makondakta kusema dakika 5 zakuchimba dawa na kuelekeza Wanaume huku na Wanawake Kule bila kujali katika basi kuna watu na wakwe zao na watu na watoto zao nasema sipendi kuona.

Pia nauliza serikali ya mkoa wa Morogoro kuruhusu wafanyabiashara ya nyama choma na chakula kufanyabiashara eneo la Sokol la miwa barabara kuu ya Morogoro - IRINGA bila kuweka kuweka maji japo kuna Vyoo vipya eneo hilo ni kukaribisha ugonjwa wa kipindupindu kwa wasafiri? Nasema kuu wa mkoa wa Morpgoro na wakuu wa wilaya pamoja na mabwana afya spendi Kabisa tabia hiyo

Mwisho nawaomba viongozi zingatieni uhifadhi na utunzaji wa mazingira acheni kuruhusu mazingira kuchafuliwa ovyo na madereva na wachimba dawa wao.

Ni ushauri wangu mpita njia Francis Godwin

0 Maoni: