January 25, 2012

TUMEUMBUKA,BASI LA ABIRIA BILA MIKANDA KTK SITI ASKARI WA USALAMA BARABARANI WA NINI?

Kumbe basi la kisasa nililopanda Leo halina mikanda katika siti ?basi hili ambalo linafanya safari zake Kati ya Tanzania na Malawi ni la kisasa kweli kwa nje ila ndani hakuna siti ya ABIRIA yenye mkanda.

Asubuhi nikiwa katika stendi ya ubungo niitaka kufunga mkanda sikuona nikajua ni siti yangu pekee ila baada ya kufika mkoa wa Morogoro askari wa usalama barabarani ametufumbua baada ya kutaka abiria wote tufunge mikanda kila moja ametazama katika siti yake bila kuona mkanda.

Ila hakuna hatua zilizochukuliwa kwa basi kukosa mikanda.

Je tujiulise sasa mabasi ya abiria kuendelea kufanya safari bila kuwa na mikanda katika siti Kama kinga kwa abiria wakati wa ajali askari wa usalama barabarani wanatimiza wajibu wao?

0 Maoni: